HIZB UT-TAHRIR AFRIKA MASHARIKI YATOA RAMBI RAMBI KWA MSIBA WA KUZAMA   KWA MELI.

Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki imepokea kwa huzuni na masikitiko makubwa taarifa ya kuzama kwa meli ya Spice Islander iliyotokea usiku wa kuamkia leo tarehe 10/09/2011 katika eneo la mkondo wa Nungwi baina ya kisiwa cha Pemba na Unguja, na tunaungana na walioathirika kuwafariji kwa msiba huu na kuwataka wawe na subra katika kipindi hiki kigumu.
Aidha, tunatangaza kwa ulimwengu wa kiislamu kwamba una wajibu kwa haraka kusaidia katika uokozi na kuzisaidia familia zilizopotelewa na ndugu ambao ni nguvu kazi ya familia hizo.
Ajali hii ni kielelezo wazi ziada cha kushindwa kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kutoa usafiri wa uhakika baina ya kisiwa cha Unguja na Pemba pia kushindwa kwa mamlaka zake husika kusimamia vyema usalama wa abiria na uokozi.
Wakati Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki tukiwafariji kwa subra na ustahamilivu wote walioathirika, pia tunatamka wazi kwamba ni dola ya kiislamu ya Khilafah pekee ndio yenye dhamira ya kweli na ya kimaumbile katika kulinda na kuokoa maisha ya watu.
Masoud Msellem
Naibu Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki

0 comments:

 
Top