TAASISI YA VYOMBO VYA HABARI KUSINI MWA AFRIKA–TAWI LA TANZANIA (MISA-TAN) INAPENDA KUWATANGAZIA WANACHAMA WAKE KUHUSU MKUTANO MKUU WA MWAKA NA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA ASASI HIYO.
MKUTANO HUO UTAFANYIKA KATIKA UKUMBI WA RUSSIAN CULTURAL CENTRE, UPANGA SEA VIEW, SIKU YA JUMAMOSI SEPTEMBA 10, 2011 KUANZIA SAA 3.00 ASUBUHI
AGENDA1. Ufunguzi na Kuhakikisha “quorum”
2. Kuridhia Ajenda
3. Kuthibitisha kumbukumbu za mkutano uliopita
4. Yatokanayo
5. Kuwasilisha na Kupitisha Ripoti ya Mwaka 2010/2011
6. Kuwasilisha na Kupitisha Ripoti ya hesabu za Mwaka 2010/2011
7. Uchaguzi wa Viongozi
8. Mengineyo
9. Kufunga mkutano
Wanachama wote hai wanakaribishwa kuhudhuria.
Wale wote wanaotaka fomu za kugombea uongozi katika Baraza la Uongozi la Taifa (NGC) kwa mujibu wa katiba ya MISA-Tan wanatakiwa kuchukua na kurudisha fomu hizo kabla ya tarehe 2 Septemba 2011. Ofisi ya MISA-Tan haitapokea fomu yoyote baada ya tarehe hiyo. Nafasi za kugombewa ni pamoja na Mwenyekiti, Mjumbe mmoja mwenye taaluma ya sheria, Mwekahazina ambaye atakuwa na sifa za uhasibu na wajumbe sita wa NGC. Wajumbe hao sita watachaguliwa kulingana na kanda (kama Katiba ya MISA-Tan ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2007).
Kanda hizo ni Zanzibar,Kanda ya Mashariki (DSM, Morogoro, Pwani, Mtwara na Lindi),Kanda ya nyanda za Juu Kusini (Iringa, Mbeya, Rukwa na Ruvuma), Kanda ya Ziwa (Shinyanga, Kagera, Mwanza, Mara na Kigoma) Kanda ya Kati (Dodoma, Singida na Tabora) na Kanda ya Kaskazini (Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga). Wagombea wote na wapiga kura wanatakiwa kuwa wanachama kwa kipindi kisichopungua miaka miwili.
Ukisoma tangazo hili mtaarifu na mwenzakoNB: FOMU ZIWASILISHWE OFISINI KWETU CLOCKTOWER SHOPPING CENTRE GHOROFA YA KWANZA CHUMBA NAMBA 2 , MTAA WA UHURU/NKRUMAH AMA KWA BARUA PEPE.
IMETOLEWA NA
ANDREW MARAWITI
KAIMU MKURUGENZI
0 comments:
Post a Comment