Ni muda mwafaka kwa kizazi hiki ya sayansi na teknolojia kuweza kufanya mabadiliko makubwa kwatika suala zima la haki na wajibu kwa mtoto, ingawaje hili ni jambo gumu kutekelezeka na ni kikwazo kikubwa kwa baadhi ya watu kutokana na mazoweya na mila iliorithiwa kutoka kwa mabibi na mababu katika karne zilizopita.
Ingawaje mwanadamu kutokana na halia alaivyo anapenda sana kuishi kwa mazoweya lakini anapopelekea suala zito kama hili la kubadilisha tabia ya kuwajali na kuwaheshimu watoto kwake bado inakuwa ni kikwazo na kutaka kujuwa tangu lini mtoto akawa na haki kama alivyo yeye mtu mzima.
Ipo jamii inayodhani kwamba mtoto ni sawa na punda kwamba kila jambo baya anastahiki apowe yaye lakini binadamu huyo huyo anasahau kwamba naye alitokanana na utoto na sasa amekuwa mtu mzima wa kuitwa baba au mama, hebu tuangalie athari zitokana na kutowatendea haki watoto, kwa mfano jamii ya sasa imekuwa haioni aibu wala fedha pale ambapo mtu mzima mwenye akili timammu kumbaka mtoto wa mika miwili, mitatu n.k hii ni kutokana na ukosefu wa kutokuwepo na sheria madhubuti za kumlinda na kumuhifadhi mtoto kama zilivyo sheria za kumlinda mtu mzima.
Kama hayo hayatoshi wapo pia wanaodiriki kuwapa mimba watoto wa miaka kumi na kumi na tano ambao kwa njia moja au nyingine wanaweza wakawa ni wanafunzi au ni mjuu wake halisi jee hali hii ya manyanyaso kwa watoto itaendela hadi lini?
Athari nyingine itokanayo na mimba hizo za umri mdogo ni kuzalisha idadi kubwa ya watoto wa mitaani ambao kwa ujumla hawana mtu au taasisi ya kuweza kuwahudumi watoto hao.Ipo haja kwa jamii kuhemuheshimu mtoto kwa vile naye anahaki ya kuishi kama ilivyo haki ya kiumbe kingine hapa duniani, wito wangu kwa jamii na taasisi zinazotete haki za binadamu kusini na mashariki mwa Afrika kuwa makini katika kutetea haki za watoto badala za mwanamke peeke yake

0 comments:

 
Top