Ipo haja kwa vyombo vya habari vya kijamii kuhakikisha kwamba vinaanda na kuratibu vipindi bora ambavyo vitaweza kusaidia jamii na hasa ya wanawake ambayo inaonekana ipo chini kiuchumi, kisiasa na kijamii. Kwa hakika vipindi bora vya radio jamii n.k zina nafasi kubwa katika kuhakikisha kwamba jamii inabadilika kutokana na mifumo mibovu ambayo kwa njia moja au nyengine zimekuwa zikidumaza maaendeleo ya wanawake nchini kwa visigingizio tofauti kama vile dini, mila na desturi za kabila fulani.
Wapo wanaodhani kwamba mwanamke si chochote si lote kutokana na mila, silka na tamaduni zao ambazo kwa hakika kwa njia moja au nyengine sheria na tamaduni hizi kandamizi zinakwenda kinyume na matakwa halisi ya sheria za nchi na dini.
Si dhani kwamba ipo dini hapa duniani ambayo inamkosesha haki mwanamke kumiliki au kufanya kitu ambacho ni cha maaendeleo, lakini wapo watu ambao wamekuwa wakitumia mgogongo au bazia la dini kwa kufanya vitendo vya hujuma kwa mwanamke asiendelee kiuchumi, kisiasa na kijamii.
Ingawaje zipo kauli mbio au maoni tafauti ya kuwawezesha wanawake kiuchumi lakini njia zote hizo bado hazitowi fursa ya kumfanya mwanamke wa Tanzania kuweza kuendelea na kujielewa yeye ni nani na wajibu wake ni nini katika jamii na ujenzi wa taifa lake.
Kwa maana hiyo basi maneno ya wanawake wakiwezeshwa wanweze haya bado hayajawa na mantiki yoyote muhimu ambao inawafanya wanawake wawee kujikombo kiuchumi, kisiasa na kijami bali kauli hii inawafanye wanawake waendelee kuwa wategemezi kutoka kwa watu wao wa karibu(wahisani), mashirika binafsi, vyama vya kisiasa n.k



0 comments:

 
Top