Mashirikiano kati ya jumuiya Uhifadhi ya Mji Mkongwe pamona na taasisi zisizo za kiserikali na zile za kiserikali ni jambo la muhimu kwani huwaweka watu waishi ndani ya mazingira ya mji mkongwe wa Zanzibar kuendelea kubakia katika orodha ya miji iliyomo kawenye urithi wa ramani ya dunia
Waziri wa Habari Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar, Mhe Abdallah Jihadi Hassan alisema kwamba jamii yote ya Zanzibar infahamu kwamba Mji Mkongwe ndio mji pekee kwa uapande wa Zanzibar ambao upo kwenye orodha ua urithi wa duni hivyo ni vyema kila mwananchi awe na ufahamu mzuri kwa kuulinda na kutunza kumbuku na tamaduni zilizomo ndani ya mji mkongwe kiwe ni kielezeo tosha kwa vizazi vijavyo.
Mhe. Jihad alisema kuwa “ sote tunajuwa kwamba mji mkongwe wa Zanzibar umeingizwa kwenye orodha ya urithi ya miji mikongwe ambayo ndio iliyopelekea UNESCO mwaka 2000” alisema Mhe.Jihadi
Lakini mbali na hayo, Mhe, Jihadi alifafanuwa kwamba itakuwa ni faraja kubwa kwa Wazanzibar kuweza kuutunza na kuuenzi mji wao mbali ya matatizo madogo madogo yanayojitokeza ambayo kwa sasa yanahitaji ushirikiano kati ya jumuiya zisizo za kiserikali kama hii ya Uhifadhi wa Mji Mkongwe kwa kuweza kushirikiana na Serikali katika kutafuta mbinu bora za kuweza kulinda na kuuhifadhii mji mkongwe usijeukapoateza hadi yake




0 comments:

 
Top