Ni hivi karibuni  duniani kote kulifanyika maadhimisho ya siku ya waandishi wa habari duniani na hapa Tanzania yalifanyika karibu kila pembe ya nchini na kila mtu aliweza kutoa maani yake juu ya maadili ya habari, upatikanaji na utoaji wa habari pamoja na upotoshwaji wa habari zenyewe
Si rahisi kwa mtu ambaye ufahamu wake ni mdogo kuweza kukubali kwamba kunakiasi kikubwa cha upotoshaji wa habari kwa vyombo vya ndani na vile vya nje ya nchi.
Kwa kweli ni kichekesho kikubwa na udanganyifu mkuwa uliofanywa na vyomva vya magharibi pale ambavyo walivishushia lawama vikosi vya NATO kwa kuwauwa wajuu watatu na mtoto mmoja wa karnal Mughamari Gaddaffi wa Libya kutokana na uvamizi walivyovifanya hivi karibuni katika bara laAfrika.
Mara baada ya kuona lawama zimekuwa nyingi katika mataifa hayo yaliyofanya uvamizi nchini Libya ndipo uongo ukatungwa na vyomba vya habari kuchukuwa nafasi ya kutangaza uongo huu kwa kudai ati Osama bin Laden ameuliwa na vikosi vya marekani na mwili wake kuzikwa baharini maana amekuwa samaki ambaye hufa baharini na kuzikwa baharini ila samaki wakati mwengine huliwa na binadamu
Kichekesho kikubwa katika igizo hili la kifo cha Osama ni kile kinachodaiwa kwamba Osama amezikwa baharini kwa sababu eti hakutakiwa katika taifa lake na jamii ya kiislam huu ni uongo wa kwanza, lakini mbaya
Kwa kweli huu ni uongo wa mwaka katika kuwanyamazisha watu wasihoji mauwaji ya Libya ambayo watu wanauliwa bila hatia, lakini kwa sababu vyombo vya habari vipo kwa ajili ya kuwadanya wananchi ndio maana watu wote duniani wameamini kwamba kilichofanyika Libya si tatizo bali tatizo ni kifo cha anaedaiwa kuwa ni Osama bin Laden.
Lakini hebu tujielieze Osama huyu amekufa mara ngapi? Kwa sababu kwa mara ya kwanza kifo cha Osama kilitangazwa mwaka 2000, mara ya pili 2005 na sasa ni mara ya tatu 2011 na pengine 2015 atakufa tena, hili linawezekana.
Ingwaje sherehe za uhuru wa vyombo vya habari ni sherehe za kimataifa lakini kwa waandishi wa mataifa ya magharibi sherehe kubwa ni kuipotosha jamii juu ya suala zima la Libya na Osama kama vile ilivyokuwa kwa Sadamu Hussein na silaha za nyuklia kule Iraq.
Uongo huu wa waandishi wa habari hata Yesu (Issa bin Mariam) alikwisha utanabahisha zamani kwenye biblia “ Mtakapo washinda waandishi na mafarisayo ufalme wa Mungu mtaupata” aya nyingine ni “Sikuja kutenguwa taurati lakini tazama kalamu zenye uongo za waandishi zimeifanya taurati ya bwana kuwa ni UONGO” hizi ni aya mbili ambazo kila moja imekuwa ikisisitiza kuhusu suala zima la waandishi na sasa tunawaita waandishi wa habari
Ingawaje wa si rahisi sana mtu kuweza kukubalia na hilo lakini ipo haja kwa mwanadamu yoyote ambaye ufahamu wake upo makini kuweza kujiuliza mara kwa mara hivi Osama kama lini na wapi? Kwa sababu kama ndugu msomaji utawakuwa uanafuatiali kwa makini, hata hao Wanaomuogopa Osama wamekuwa wakitofautiana kimawazo na taarifa, kuhusiana na kifo cha Osama bin laden ambae inasadikiwa kuwa ni miongoni mwa viongozi muhimu katika kundi lake
Si jambo la kushangaza sana kuhusu siku hii muhimu kwa wanahabri wote unia, badala ya kuadhimisha siku yao ya UHURU WAVYOMBO VYA HABARI kinyume chake, waandishi wa habari karibu duniani kote waliadhimisha siku hiyo kwa kuandika habari za kifo cha Osama ambaye mpaka sasa hakuna ushahidi wakutosha kama kweli kafa au la? Hii ni kutokana na taarifa zenywe zilivyo na umuhimu wa Osama kwa taifa la Marekani iweje mtu ambaye anatafutwa kwa uvumba na udi akamatwe na kuuwawa bila ya kuonesha picha halisi la tukio lenyewe, hii haingii akilini kwa sababu hata walipomkamata Sadam Hussein walimuonesha hadi siku waliyomnyonga, lakini kwa Osama bado ni kitendawili kizito ambacho kwa kweli hakina muaguzi.
Si tu kwamba kitandawili hicho kimekosa mtu wa kukiaguwa bali kichekesho chengine ni kile kuripotiwa kwa ushahidi wa DNA za Osama ambzo pia hukuwa na jibu sahihi juu ya taarifa za uhunguzi wa damu hiyo hatukatai kwamba wenzetu wapo mbali kwa taaluma hiyo lakini, kama ni kweli taarifa hizo za uchunguzi wa DNA zilipaswa kutolewa malezo na Daktari aliyehusika, hospitali na vitu vyengine kama hivyo, lakini leo hii Muandishi wa habari alisimama na kuwa Daktari na kushindwa hata kuhoji kulikoni?
Kwa kweli yapo masuala mengi sana ya kujiuliza juu ya kifi hicho na uhuru wa vyombo vya habari lakini kwa upande mwengine wa shilingi hapa nchini napo kumekuwa na kizazaa kikubwa cha kuifumba macho jamii ya Kitanzania na hasa katika masula muhimu ambayo kwa kiasi fulani yamekuwa yakiitikisa serikali ya Tanzania kama vile Wizi na Ubadhirifu wa Mali ya ummah ( ufisadi) yote hayo kwa njia zile zile ambazo vyombo vya habari vya magharibi wamekuwa wakitumia kuwazuga wananchi, lakini kwa Tanzania haikuwa Osama bin Laden kwani alikuja kabla lakini kwao si kitu kingine bali BABU WA LOLIONDO na tiba yake ya kikombe
Ni kihekesho jamii ambayo inahitaji kufahamu ukweli juu ya matumizi halali na nini kinachoendelea bungeni matokeo yake wamekuwa wakimbia tiba ya babu na sasa kuna uwezekano wa kutumia fedha kwa ajili ya ujenzi wa kumuwezesha babu kutoa tiba hiyo ipasavyo. Kuna haja ya kujiuliza kwa kupitia huu uhuru wa vyombo vya habari na upatikanaji wa habari zenyewe, hivi ujenzi ambao unafikiriwa kule Loliondo ni wa kudumu au ni wa muda? Hii ni kwa sababu mtoaji ndawa ni mtu mmoja tu na si zaidi ya hapo kwa mojibu wa tarifa zilizokuwa zikisomwa na kuchapiswa kunywe vyombo vya habari tofauti nchini. Jee Mungu akichukuwa amana yake (kufa kwa babu) hayo majengo yatafanyiwa nini? Yatakuwa magofu ya kihistoria? Nyumba za kukaa wanyama? Ndege au maharamia? Haya ndio masuala muhimu ya kujiuliza kabla ya ujenzi kuanza huko Loliondo kwani nahofia fedha zinaweza zikatumika nyingi halafu majengo yakabakia kuwa ni vihame visivyofaa
Si kama napingana na ujenzi huu wa kuimarisha majengo ya tiba huko Loliondo, bali ninachokiangalia ni ule ujenzi wamajengo ya kudumu katika eneo hilo wakati Babu mwenyewe amekwisha toa tahadhari kwamba hakuna mtu mwengine ambaye anaweza kutengeneza wala kutoa dawa hiyo ispokuwa ni yeye peke yake, lakini kunamabadiliko mengine basi ni vizuri kwa ajili ya kuwasaidia wananchi katika kupata tiba hiyo ya jadi
Ipo haja kwa jamii pia kuweza kufahamu umuhimu wa vyombo vya habari nchini, ingawaje wapo wanaodhani kwamba vyombo hivyo vipo kwa ajili ya Serikali na wanasiasa tu, kwa kweli hayo siyo mawazo sahihi na ipo haja ya kuweza kufahamu kwamba vyombo vya habari vipi kwa kila mtu ambaye yupo tayari kutoa taarifa ambazo ni za kweli na ni sahihi si kama zile a kifo cha Osama ambaye taarifa zake zimekuwa zikikhitilafiana kila wakati zipo taarifa za kufa kwa osama kwama 2000,2005 na sasa 2011 na pengine 2015 anaweza kufa tena


0 comments:

 
Top