Suala la tiba ni kitu muhimu kwa kila mwanadamu na nndio maana Serikali imekua ikitafuta kila njia katika kuhakisha kwamba raia wake wanaishi katika hali ya afya njema
Ingawaje kwa sasa kila mtu ambaye anaishi ndania ya Mipaka na nje ya mipaka ya Tanzania utakapomuuliza kuhusu Arusha hapana shaka yoyote atakwambia kuhusu Babu wa loliondo ambaye ndio kwa sasa amekuwa ndio kioo na tengemeo la wakaazi wengi wa Tanzania na hii inaonekana kwamba wananchi wengi wa Tanzania ni wongonjwa na hawana tiba rasmi na ndio maana wameamuwa kwenda Loliondo
Si vibaya mtu kutafuta njia muafaka kwa ajili ya kujipatia tiba, lakini kitu cha msingi kwa mujibu wa sheria za Tanzania ni kwamba mtu au taasisi yoyote ile ambayo itakuwa inataka kutoa tiba ni lazima iwe imesajailiwa kisheria, kinyume chake babu wa Loliondo hada sasa sidhani kama atakuwa amesajiliwa rasmi katika wizara husika ambayo ni Wizara ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchini suala ni kwamba jee Bubu wa loliondo amesajiliwa wapi?
Ingawaje suala hili lipo zaidi katika imani za kidini, si dhani kama ni sahihi, lakini suala la kujiuliza jee kupitia dini ndio kigezo cha kuvunja sheria?

0 comments:

 
Top