Walimu wanne kutoka katika Chuo cha Muziki Zanzibar,wameondoka nchini na terehe 7.10.2010 na kuanza safari ya kuelekea katika kisiwa cha Mayotte(Comoro) kwa ajili ya kuendesha mafunzo ya taraab asili kisiwani humo.
Mafunzo hayo yamefadhiliwa na Idara ya Utamaduni ya Mayotte imeanza rasmi tarehe 7 mwezi huu na yanategemewa kumallizika terehe 25.10.2010, ambapo mafunzo hayo yataendeshwa na walimu Mohammed Issa"Matona",Rajab Suleiman, Mohammed Othman na Kesi Juma, ambapo walimu hao watafundisha jinsi ya kutumia (kupiga) Udi, Filda(Violin) na Qanun.

0 comments:

 
Top