wauguzi katika kituo cha afya ni watu muhimu sana katika jamii na hasa ukizingatia kwamba ni kazi ya wito au kujitolea zaidi
ukiangalia kwa makini hii ni kazi ngumu kwa mtu wa kawaida, kwa sababu si kila mtu anaweza akawa muuguzi au daktari, kwani ili awezekuwa daktari ni lazima apatiwe taaluma ya fani hiyo
kwa kuwa hii ni kazi ya wito na ni hiyari ya mtu binafsi, basi ni lazima nidhamu iwepo katika utowaji wa hudumakwa jamii, kwani kuwepo kwake pale hospitali ni kwa ajili ya kuisaidia jamii na si vyenginevyo kama hawezi ni bora atafute jembe akalime
ni kinyume na matarajio ya wengi wafikapo katika vituo vya afya,kwani mara nyingi watu wafikao katika vituo vya afya huambalia matusi na dharau kutoka kwa wauguzi ikiwa ni pamoja na kuendekeza ubinafsi wa utoaji wa huduma hiyo kwa baadhi ya wateja, kwani maranyingi huduma bora za afya hupatikana kwa udugu na hisani ya mtu fulani
lakini kwa wauguzi wangi hapa nchini wemekuwa na tabia ya dharau kwa wagonjwa na inafika muda mgonjwa anajuta kwenda hospitali kwa kuhofia masimango na matusi ya baadhi ya wauguzi nchini
kwa kiasi fulani inaonekana kama kwamba haya matusi ni miongoni mwa mitaala yao kule chuoni, kwa si hivyo kwani wanashindwa kuwa na nidhamu?. Zanzibar mara nyingi watu huwa wanalalamika zaidi vituo vya Serikali kwa ni vituo pekee vinavyotoa huduma kwa unafuu na hukusanya watu wengi kwa wakati mmoja
kwa mfano, unapokwenda katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja, takribani kila kitengo kimekuwa na matatizo yake, zipo sababu tofauti kama vile za kiutendaji n.k, lakini bdo suala la matumizi ya lugha bora imekosekana karibu vitengo vyote
kitu cha msingi ni kujiuliza wewe dakatari au muunguzi ambaye upo katika kituo cha afya upo hapo kwa faida ya nani? na pia unatakiwa ujiulize kuna mtu yoyote aliyekulazimisha kufanya kazi hiyo au nini wewe mwanyewe ndie uliyeichanguwa? kwa kuweza kuyajibu maswala hayo ndio utaweza kutoa huduma nzuri na kuwaheshimu wateja wako
0 comments:
Post a Comment