Kampuni ya ujerumani ya kimataifa Bosch Group imesimamia mkutano wa kwanza wa kimataifa ambao umezindua meza ya majadiliano kuhusu uchakataji na ufungaji wa kahawa siku ya Ijumaa katika Addis Ababa nchini Ethiopia .

Mkutano huu umekusanya wawakilishi kutoka Shirika la Maendeleo ya Viwanda la Umoja wa Mataifa (UNIDO), taasisi kadhaa za viwanda na za kilimo, biashara kubwa, kampuni ndogo na za kiwango cha kati, wakulima, vyama vya kiraia pamoja na mashirika ya misaada ya ndani na ya kimataifa katika jitihada za kimkakati kwa ajili ya kuboresha usalama wa chakula.

Lengo la mjadala huu limekuwa kuzidisha utambuzi wa maeneo kwa ajili ya kuboresha usalama wa chakula katika kanda na kufikiria wakati huo huo jinsi gani kuongeza ubora wa maisha kwa wananchi kupitia kukuza ukuaji wa kiuchumi katika mojawapo ya sekta muhimu za nchi. Na zaidi mjadala huu umekusudia kukusanya wadau muhimu kwa kuchukua hatua ya kwanza kwa ajili ya kuongeza thamani ya ziada na ujenzi wa viwanda ndani ya nchi.

Ethiopia inaaminika kuwa mahali pa kuzaliwa pa kahawa (tafadhali tazama Karatasi ya habari iliyoambatishwa) ambapo sasa hivi mmoja katika kila raia watano anahusika katika sekta hiyo.

Baraza hili lilifanyika wakati wa Maonyesho ya tatu ya kila Mwaka ya Addis Agrofood iliyofanyika tarehe 27 hadi 29 Novemba 2015. lilisimamiwa na divisheni ya biashara ya kikundi cha Bosch, Bosch Packaging Technology, ambacho ni kiongozi wa soko la kimataifa.

Miongoni mwa mada zilipojadiliwa ni pamoja na njia za kutosha za kuongeza usindikaji na ufungaji kahawa kwa ajili ya masoko ya ndani, ya kikanda na masoko ya nje na ya rejareja.

Vitu vingine vilivyojadiliwa ni pamoja na teknolojia ya kisasa kuhusiana na kukaanga na pia kwa ajili ya wakuzaji wa kahawa pamoja na ufumbuzi wa kiufundi kwa ajili ya ufungaji endelevu.

Bosch Packaging Technology ina mashine za ufungaji zinazotumia nishati kwa ufanisi karibu laki na thelathini (130 000) ambazo zimesimikwa na kutumika katika viwanda elfu kumi na tatu (13 000) duniani kote. Inapatikana katika nchi mia na sabini (170) pamoja na sifa yake ikiwa ni pamoja na aina mbalimbali za mashine mia mbili hamsini (250) katika sekta ya biashara arubaini (40).

Utamaduni wake wa kufanya biashara kwa ufahamu ulisababisha kampuni hiyo kushiriki katika kiupaumbele cha "Kuhifadhi Chakula" cha Umoja wa Mataifa tangu mwaka 2011. Mpango huu unalenga kutafuta ufumbuzi juu ya matumizi mabaya na kupoteza chakula ulimwenguni na kuhakikisha kuwa chakula kidogo kipate kupotea njiani kikielekea kwa wateja na katika mikono ya wateja wao wenyewe.

Kama kiongozi wa soko, Bosch Packaging Technology inaruhusu chakula kusafirishwa kwa ubora zaidi kwenye mastafa mrefu kwa watumiaji wa mwisho katika masoko yanayoibukia.

Dk Markus Thill, Mkubwa wa Bosch Afrika, alisema mwaka 2013 Bosch Packaging Technology ilipokea maombi elfu sabini na saba (77 000) ya kimataifa peke yake, akielezea: "Kama sehemu ya kikundi cha Bosch tunatoa kiwango bora cha teknolojia ambazo zilibuniwa kwa kudumu katika maana halisi. mashine zetu, ufumbuzi wetu na huduma zetu zinatoa msaada muhimu kwa afya na lishe ya binadamu - hasa katika masoko yanayoibuka kama vile zile katika Afrika".

Aliongeza ifwatayo: "Na mashine zetu ni imara, inayodumu kwa mda mrefu, rahisi kutumia na inayojivunia matumizi madogo ya nishati. Ndio maana tunaamini kwamba pamoja na wadau muhimu tunaweza kusaidia na kuwezesha maendeleo ya sekta ya kahawa nchini Ethiopia ."

Kama kiongozi wa soko, Bosch Packaging Technology inaruhusu chakula kusafirishwa kwa ubora zaidi kwenye mastafa mrefu kwa watumiaji wa mwisho katika masoko yanayoibukia.

Ethiopia ni mhusika kubwa katika soko la kahawa duniani. Kwa sasa ni mzalishaji wa sita mkubwa zaidi duniani, ikisafirisha tani zaidi ya laki na hamsini (150 000) kwa mwaka. Hata hivyo, nchi husafirisha nje zaidi ya asilimia tisini (90%) ya bidhaa zake mbichi na isiyokobolewa, haijasindikwa na haijafungwa. Hii ina maana kwamba idadi kubwa ya faida inatoka nje ya nchi.

Sasa Bosch Packaging Technology inachukua mstari wa mbele katika kuendeleza ushirikiano binafsi wa uma ili kujenga mazingira mazuri kwa wajasiriamali na wakulima kushiriki kikamilifu katika viwanda kupitia usindikaji, kukaangwa, utengenezaji,ufungaji na hata kusambaza kahawa mbichi.

Bwana Vandan Rughani, Mkurugenzi Mtendaji wa Bosch Afrika Mashariki aliendelea kusema: "Tunaamini kwamba teknolojia ni njia bora ambayo sekta ya kahawa inaweza kupiga hatua mbele huo mlolongo wa thamani nchini Ethiopia na kushindana kimataifa.

ndio maana UNIDO inatumika na makampuni kama Bosch ili kuifamya kuwa halisi. Bosch huupitia mpango huu kama muhimu kwa maendeleo ya bara la Afrika pamoja katika suala la maendeleo ya kiuchumi na endelevu kama vile kuimarisha usalama wa chakula. Ushirikiano kama mfano wa biashara yetu inazidishwa kwaa kuunda mda-mrefu, ufumbuzi endelevu wa kujitokeza na kuendeleza masoko. "

Alisema kuwa meza ya mazungumzo ni haswa hatua ya kwanza ya kuhakikisha Ethiopia inazidisha rasilimali ya kahawa ya nchi kwa ajili ya maendeleo zaidi ya kiuchumi wa kijamii.

"Kilimo kimewekeza kwa karibu nusu ya pato la taifa ya nchi hiyo (GDP). Aidha, Ethiopia ni miongoni mwa nchi za afrika ambayo uchumi wake unaongezeka kwa kasi na sasa ni wakati wa kuchochea tija yake ndogo au pana ya uchumi itakayofaidi watu wake wote. Na teknolojia inasaidia katika suala hili."

Bosch ni wasambazaji wa kimataifa wanao ongoza kwa teknolojia na huduma za kazi katika nchi zaidi ya mia na hamsini (150) na kuajiri zaidi ya laki tatu na sitini (360 000) kupitia matawi yake mia nne na arobaini (440) na maslahi ya kikanda. Kinachofanya mtindo wa biashara yake kuwa wa kipekee ni kwamba asilimia tisini na mbili (92%) ya kampuni inamilikiwa na shirika la mhisani. Hii uhakikisha kwamba, bila ya kushinikizwa faida, mtazamo wake ni katika kubuni ufumbuzi endelevu wa kimataifa kwa njia ya uwekezaji mwangalifu.

Dr.Thill:.. "Teknolojia inapatikana kwa wajasiriamali wa ndani na wakulima ili kuboresha usalama wa chakula, kutokomeza upotevu na kujenga viwanda vipya. Tayari tumeisha kuanza kusambaza mashine za ufungaji kwa wenyeji wa biashara na wakulima na vyama vya ushirika. Hii inawaruhusu kusindika na kufunga kahawa ndani na hivyo kuinua ukuaji katika mzunguko wa thamani."

Bwana Vandan Rughani ametoa kauli kwamba: "Tunaamini mfumo wa jumla itakuza kampuni ndogo na za kiwango cha kati, kuchochea ubunifu wa kazi kama vile fursa za nyongeza na viwanda vya ziada zaidi chini ya mzunguko wa thamani."

Distributed by APO (African Press Organization) on behalf of The Bosch Group.

0 comments:

 
Top