Ujumbe wa mawaziri na viongozi wakuu kutoka nchi za Afrika Mashariki wameahidi kuunga mkono harakati za kutafutia umwafaka tatizo la upungufu wa nishati.
Mhe. Joseph Njoroge, Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati, Kenya, Mhe. Christopher Yaluma, Waziri wa Nishati na Madini, Zambia, Mhe. Waziri James Musoni, Waziri wa Miundo msingi, Rwanda na Bi. Maria Kiwanuka, Mshauri Mkuu wa Mhe. Rais na afisa katika ofisi ya Wizara ya Fedha nchini Uganda watasaidiwa na viongozi wenye usemi katika sekta ya kibinafsi ya nishati katika kikao cha Nishati Afrika Mashariki kitakachofanyika Machi 25-27 jijini Nairobi kuangazia dharura ya mgogoro wa kusambaza nishati.
Wazungumzaji muhimu kutoka Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), IFC, Barclays, Symbion Power, KenGen, KPLC, UMEME na EEP watahutubu kuhusu hatua zinazoweza kuleta mabadiliko katika sekta ya nishati ikiwa ni pamoja na; nafasi muhimu ya usambazaji umeme katika mchakato wa kuendeleza viwanda, umuhimu wa nishati, jinsi ya kukabiliana na vizuizi vya mikopo na jinsi gharama ya mikopo katika kanda inaweza kupunguzwa kwa kuimarisha usambazaji umeme.
Meneja wa Mpango wa EnergyNet Bi. Ms Veronica Bolton-Smith alizungumza kuhusu hatua ya Mawaziri kukubali mialiko; “Ukizingatia kwamba mkutano huu unalenga washirika wachache, uwepo wa vigogo wanne katika sekta ya kibinafsi ya nishati katika kanda hii ni ishara ya haja ya kuwa na mdahalo wenye lengo.”
Distributed by APO (African Press Organization) on behalf of EnergyNet Ltd
0 comments:
Post a Comment