Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi anaondoka Nchini leo jioni kuelekea chini Jamuhuri ya Watu wa China kwa ziara ya Kiserikali ya siku kumi yenye lengo la kuimarisha uhusiano wa muda mrefu kati ya China na Zanzibar.
Balozi Seif anayeuongoza Ujumbe wa Viongozi wanane wakiwemo mawaziri, Makatibu wakuu pamoja na watendaji waandamizi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ataanzia ziara yake katika Kisiwa cha Jimbo la Hainan kiliopo katika ncha ya kusini mwa China.
Katika ziara hiyo Makamu wa Pili wa Rais aliyeambatana na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi anafuatana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Vijana Mh. Said Ali Mbarouk, Waziri wa Ardhi, Makazi, Maji na Nishati Mh. Ramadhan Abdulla Shaaban, Meya ya Manispaa ya Zanzibar Msitahiki Khatib ASbdullrahman Khatib na Mwakilishi wa Jimbo la Chaani Mhe. Ussi Jecha Simai.
Wengine ni Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Dr. Khalid Salim Mohd, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Nd. Khamis Mussa Omar, Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum Nd. Joseph Abdulla Meza, Katibu Mkuu Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Nd. Julian Banzi Raphael, Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Nd. Abeid Juma Ali pamoja na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitega Uchumi Zanzibar { ZIPA } Nd. Salum Khamis Nassor.
Katika ziara hiyo Balozi Seif na Ujumbe wake anatarajiwa kuufungua Mkutano wa Tano wa Kimataifa wa Mashirikiano baina ya Viongozi wa Bara la Afrika, Mabalozi wa Mataifa ya Bara la Afrika waliopo Chini China pamoja na Wawekezaji wa Jimbo la Hainan.
Makamu wa Pili wa Raia wa Zanzibar atapata fursa ya kutembelea maeneo ya uwekezaji katika Kisiwa cha Hainan ikiwemo Viwanda vya kusindika samaki, maeneo huru ya Uwekezaji haliyopo katika Mji Mkuu wa Hainan Haikou, kiwanda cha kusindika nazi na maji ya madafu.
Ziara hiyo ya Balozi Seif na Ujumbe wake pia itamuwezesha kukutana na wenyeji wake wa Kisiwa cha Jimbo la Hainan pamoja na kuitembelea Bandari kubwa ya Mji wa Sanya yenye uwezo wa kuhudumia Meli zenye uzito wa Tani Laki 300,000 ambayo imejengwa na Kampuni iliyoonyesha nia ya kutaka kujenga Banadari ya Mpiga Duri Zanzibar.
Balozi Seif ataendelea na ziara yake katika Mji wa Shenzhen kwa Kutembelea Makao Makuu ya Kampuni ya Kimataifa ya mtandao wa Mawasiliano ya Kisasa { ICT } ya Huawei pamoja na ile ya Mtandao wa Mawasiliano ya Kisasa ya ZTE.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Ujumbe wake anatarajiwa kumaliza ziara yake katika Mji Mkuu wa China Beijing kwa kukagua shughuli za matengenezo wa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mji huo.
Badaye Balozi Seif atakutana kwa mazungumzo na Waziri wa Biashara wa China anayeshughulikia masuala ya Afrika akiambatana Uongozi Mpya wa Benki ya Kimataifa ya Nchi hiyo Exim katika mazungumzo hayo.
Exim Bank imekuwa mshirika mkubwa kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambapo mara kadhaa imekuwa ikitoa mikopo nafuu pamoja na kufadhili baadhi ya miradi ya
Maendeleo ya Kiuchumi na Kaijamii hapa Zabnzibar.
Balozi Seif anatarajiwa kumaliza ziara yake Chini Jamuhuri ya Watu wa China Tarehe 21 Novemba kwa kurejea nyumbani kwa kupitia Dubai kwa mapimziko mafupi.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
0 comments:
Post a Comment