Hapana shaka yoyote kwamba kila mtu, raia au kiongozi kubadiliko kiakili, kimtazo na matendo kwa kufahamu kwamba kila mmoja kwa nafasi yake na kwa muda tofauti anaweza kuwa mkimbizi, iwe kisiasa, uchumi, kijami au hata kimazingira hii ni sawa na kusema kwamba kila mtu ni mlemavu mtarajiwa.

Mafunzo ya isku tatu juu ya kuwa jengea uwezo waandishi wa habari katika kufahamu dhana nzima ya Ukimbizi na Uhamiaji yaliyokuwa yakiendeshwa na IOM kwa ushirikiano wa UNCHR yameweza kuwafungua macho waandishi hao kwa kuweza kufahamu tofaiti za maneno hayo pamoja na matumizi yeke.

Jamii inapaswa kufahamu kwamba mkimbisi siyo Jasusi au Muuwaji bali ni mtu kama walivyo watu wengine, ingawaje mkimbizi huwa na mahitaji maalumu kama vile watu wanaishi na virusi vya ukimwi au ulemavu ambazo haki hizo hupatiwa kwa mujibu wa sheria za nchi na zile za kimataifa.

kwa mfano yapo maneno mengi ambayo wenyeji wamekuwa wakisema juu ya wakimbizi na hasa kuhusihwa na mambo ambayo siyo mazuri na zaidi ni UOVU kama bile Ujambazi, Wizi, Unganyaji pamoja na kuisaidia kuingizi maradhi katika jamii na nchini husika, kwa ukweli jambo hilo au dhani hiyo siyo sahihi hata kidogo.

Sipendi kusema kwamba kila anayevuka mpaka wa nchi moja kwenda nyengine ni mkimbizi lakini unaweza ukawa mkimbi wa ndani ya taifa lako hii ni kutokana na sababu mbali mbali zikiwemo za uchumi, kisiasa, kiuchumi, kijamii na hata kimazingira yote hayo kwa njia moja au nyengine yote hayo inawezekana kuwa nido chanzo cha ukimbizi kwa kila mtu.

Katika juhudi hizo IOM na UNCHR wanapaswa kupongezwa kutoka na juhudi zao hizi za kuwakutanisha waandishi wa habari na kuwajengea uwezo katika kuhakishwa kamba kila mtu katika jamii ya Kitanzania anapatiwa elimu sahihi ya kuhusu Ukimbizi na sababu za Ukimbi ni nini.

Jamii inapaswa kuwa makini juu ya makundi yao ya kisiasa ambao kwa sasa yameanza kuonekana kuwa na ishara mbaya kwa Taifa la Tanzania hii ni kutoka na kauliza baadhi ya viongozi wa vyama vya kisiasa nchini, inawekana timiza wajibu wako.

0 comments:

 
Top